Huu Ndio Ushauri Wa Wema Sepetu Kwa Wanawake Kuhusu Wanaume
Muigizaji maarufu wa Bongo movie Wema Sepetu amewapa wanawake wenzake ushauri juu ya wanaume na mahusiano kwa ujumla.
Wema akiwa mmoja Kati ya watu maarufu Tanzania anaweza akawa anatazamwa na watu wengi kama role model kutokana na ushawishi aliokuwa nao kwa watu.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii Snapchat, Wema kaamua kuandika ujumbe maalumu ambao amewapa ushauri wanawake au wasichana katika suala zima la mahusiano ya kimapenzi ambapo Wema amewapa wanawake njia za kujua endapo mwanaume ameyachoka mapenzi na anataka kusepa.
Wema amefunguka yafuatayo:
To my ladies mwanaume akikuchoka utamjua tu….Ni visababu vya kijinga ndio vinamfanya afanye big deal….when your man starts acting up funny for no reason mpe space yake….Usimnag sana He wants space give him a football pitch…Don’t kiss azz!”.
Wema amewapa ukweli wanawake kuwa mwanaume akikuchoka kwenye mahusiano utamjua tu vitu vidogo vinakuwa vikubwa atatafuta tu kisababu kidogo ilimradi tu akununie na kama mwanamke umetambua hilo mwache mpe nafasi ya kufanya mambo yake usijipendekeze wala usimshobokee kiivooo.