Huu Ndio Ushauri Wa Mama Ashura Kwa Aslay
Mwanamuziki wa Bongo fleva Aslay Isihaka amezidi kupanda chati katika chati mbalimbali za redio na televisheni kupitia nyimbo zake zinazofanya vizuri sana kwa hivi sasa.
Mchekeshaji maarufu kutoka Timamu TV Mama Ashura amekuwa mmoja kati ya watu waliompongeza na kumpa ushauri Aslay, kupitia ukurasa wake Instagram Mama Ashura alimuandikia ujumbe huu;
“Nimeona niongee na mdogo wangu Aslay, kiukweli unafanya vyema na inaonekana unajua unachokifanya, muziki unaujua na pia kipaji unacho Big up Sana!”.
Pia aliendelea kufunguka kuwa;
“Kama ilivyotokea kwa wasanii wenye uwezo kama wako, waliposifiwa sana wakajisahau na kudhani kuwa wameshawini wakajikuta majina yamebaki juu alafu kazi zipo chini. Spirit yako nazidi kuiona kila siku nakutabiria miezi michache ijayo tutakuona kwenye level za kimataifa zaidi, lakini kuwa makini na baadhi ya mashabiki ambao sasa wanakuja kwako kwa wingi kutoka kila mahali kuna wengi ni fake fans ambao hata ukiboronga utasikia Aslay kaboronga vizuri na makofi wanakupigia badala yAslay.ukosoa ili uendelee kufanya vizuri yangu ni hayo tu naendelea kufurahia natamba bonge la songi.
Aslay anatamba na wimbo wake wa ‘natamba’ ambao kwa sasa unashika chati sana na video ya wimbo huo umempindua Diamond na wimbo wake wa hallelujah huko YouTube alipokuwa anaongoza na kwa sasa anaongoza Aslay.