Hussein Machazi asimulia alivyokutana na mchumba wake kutoka Italy

Image: Hussein Machozi

Mkali wa nyimbo za bongo Hussein Machozi hivi sasa anajikaza kufanya nyimbo ambazo vijana wanafanya na baada ya kuachia wimbo wake mpya hivi karibuni.

Hata hivyo maisha yake pia yanaonekana yamepata muelekeo mpya baada ya kupata mchumba Muitaliano. Akizungumza kwenye mahojiano muimbaji huyu alikiri kuwa hivi sasa anamchumba mbaye anapanga maisha na yeye.

download latest music    

Hussein Machozi

Hussein alisema kuwa alikutana kwanza na dadake mchumba wake huko Mombasa akipiga shoo. Na kwa sababu alipenda alivyokuwa akipiga show, msichana huyo alimuomba namba na wakaanza kuongea lakini hawakuwa na mahusiano yoyote ya kimapenzi.

Aliendelea kusema:

Ilikuwa Mombasa kwenye shoo, miaka kama mitatu hivi iliyopita, baada ya shoo akaja msichana mmoja Mtaliano akasema amependa kazi yangu, tukabadilishana namba, tukawa tunawasiliana. Baadaye yule msichana akanitambulisha kwa dada yake, tukawa tunawasiliana pia. Sasa siku moja dada mtu akamuuliza mdogo wake kama ana uhusiano wa kimapenzi na mimi, akasema hapana, basi akamwambia yeye amenipenda, tukaanza uhusiano.

 

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua