Husna Sajent Akana Tetesi za Kumpa Penzi Sholo Mwamba

Muigizaji wa Bongo movie Husna Sajenti amekana taarifa za yey kuwa na Mahusiano ya kimapenzi na staa wa muziki wa Singeli Sholo Mwamba.

Wiki iliyopita Sholo Mwamba alijitutumua na kusema amefanikiwa kumchukua mtoto mrembo Husna Sajent kutoka kwa hasimu wake nambari moja Dulla Makabila aliyekuwa mpenzi wa Husna.

download latest music    

Husna amekuwa Kwenye uhusiano na Dulla Makabila kwa kipindi kirefu hivyo taarifa za wao kuachana zilikuwa nyingi na sababu mbali mbali na Sholo Mwamba alidai moja ya sababu ni yeye maana alifanikiwa kumkwapua kutoka katika mikono ya Dulla Makabila.

Husna amekana taarifa hizo na Kwenye Interview na Enews ya East Africa ameweka wazi kuwa hana Mahusiano yoyote na Sholo Mwamba ingawa aliwahi kumtongoza:

Mimi Sholo Mwamba sio mpenzi wangu , sijawahi kutembea naye na wala haitokuja kukaa itokee atabaki kuwa mshakaji wangu tu na kama angekuwa mpenzi wangu ningesema alafu anavyokuwa ananitangazia hivyo atakuja kuniharibia Mahusiano yangu na mpenzi wangu wa sasa alafu isitoshe  ananichafulia jina mimi nakua naonekana kama kicheche fulani jambo ambalo sio kweli ajaribu kuongea ukweli”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.