Hukumu ya Babu Seya na Papii Kocha Kusikilizwa March 23
Hukumu ya Kesi ya rufaa ya mwanamuziki Babu Seya na mtoto wake Papii kocha inatarajiwa kusikilizwa March 23 kama ambavyo kesi hiyo ilikuwa imepanga ambapo wasanii hao wawili mtu na baba yake waliwahi kukata rufaa ya kukataa kutumikia kifungo cha maisha jela (kunyongwa) kwa kukutwa na hatia ya kulawiti watoto.
Mahakama ya Afrika na haki za binadamu wanategemea kuwa March 23 watasoma hukumu ya rufaa ya kesi hiyo iliyoendeshwa kwa muda kidogo huku watuhumiwa wakiwa hawajui kuwa walikuwa wanaweza kutoka kwa msamaha wa Raisi.
Babu Seya na Papii walikuwa ni kati ya wafungwa 61 kati ya 8157 waliopewa msamaha na Raisi katika sherehe za uhuru wakitumikia kifungo cha kunyongwa na hakuna aliyewahi kutegemea kuwa kesi kama hiyo ingeweza kuonekana na kutolewa msamaha na Raisi.
Raisi wa mahakam hiyo Bwana Sylvian Ore amesema kuwa hukumu ya kesi hiyo ina nafasi kubwa ya kusomwa kwa siku tajwa endapo walalamikaji watakuwa wamekamilisha masharti na vitu vinavyohitajika .
Hata hivyo baadhi ya watu walishangazwa na kuwepo kwa kesi hiyo tena ilhali watuhumiwa tayari wapo nje kwa msamaha ndipo baadhi ya mhakimu na majaji waliposema kuwa haijalishi kuhusu hali ya mtuhumiwa na mlalamikaji ila lazima hukumu isomwe.