Huddah- Nimetembea Sana na Mabilionea Lakini Sijawahi Kuwa Bilionea
Mfanyabiashara na Socialite maarufu kutoka Kenya Huddah Monroe ameibuka na jipya Baada ya kukiri kuwa ameshawahi kuwa kwenye mahusiano na wanaume mabilionea Lakini hajawahi kuwa bilionea.
Huddah amefunguka hayo Kupitia mtandao wa Snapchat ambapo ameeleza kuwa amekuwa akijihusisha kimapenzi na watu wenye utajiri mkubwa lakini yeye bado hajawa tajiri kwa sababu amegundua utajiri hauambukizwi kwa kujamiana.
Nimejihusisha kimapenzi na Mabilionea lakini sijawahi kuwa Bilionea, utajiri hauambukizwi kupitia tendo la ndoa ,inabili uwe mtumwa kwa ajili ya vitu vyako kila siku” .
Hudah ambaye Hivi sasa anafanya vyema na kampuni yake ya vipodozi ya Huddah Cosmetics ameongea hayo katika jitihada za kuwahamasisha wasichana wafanye kazi kwa bidii badala ya kutegemea kuwa na wanaume wenye pesa tu.