Hili ndilo onyo Rais Magufuli alitoa kwa wanamiliki wa vyombo vya habari Tanzania
Rais Magufuli anataka wamiliki wa vyombo vya habari Tanzania kujichunga sana wanavyo pitiza habari.
Rais alitoa onyo hilo jana, 24th March 2017 wakati akizungumza ikulu katika hafla ya kuwaapisha mawaziri wapya wawili aliowateua akiwemo Dkt Harrison Mwakyembe anayechukua nafasi ya Nape Nnauye katika wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo.
Rais alionekana kukasirishwa na venye vyombo vya habari vilivyo tilia maanani tukio lililo waslilisha waziri wa zamani Nape Nnauye na askari aliyemtolea bunduki.
“Hatuwezi tukaiacha serikali ikaangamia sababu ya watu wachache haitawezekana. Hata kasomeni tu hayo magazeti ya leo picha yote heading ni picha ya mtu ambaye alifanya kosa moja, kana kwamba hicho kitendo kimefanywa na serikali au kinasapotiwa na serikali, page ya kwanza, page ya pili, huyu anatoa anafanya hivi, huyu anafanya hivi that’s the story,” amesema Rais.
“Nawaambia wamiliki wa vyombo vya habari be careful and watch it. Kama mnafikiri mna freedom ya namna hiyo not to that extent,” alionya.
Rais Magufuli amekuwa akisisitiza vyombo vya habari vipee maswala ya kimaendeleo kipao mbele na sio maswala ya kuleta uchochezi tu.