Hili ndilo jambo RC Makonda alipiga marufuku kutokea jana, 6th April 2017 pale Dar es Salaam
Wasanii na wasambazaji wa filamu Tanzania walitua kwenye ofisi ya RC Makonda wakiwa na malalamiko mengi. Walidai ya kwamba hawanufaiki na kazi zao za filamu kutokana na kuwepo kwa maharamia wanaoziiba kazi hizo kwa kuzi-download kisha kuzisambaza kimagendo kwa bei ya kutupa bila ridha yao na zikiwa hazina stempu ya mamlaka ya mapato.
Kwa hilo RC Makonda alichukua hatua hapo hapo kupiga marufuku kuanzia Alhamisi hii tarehe 06 Aprili, 2017 uuzwaji, uingizwaji wa filamu za nje ambazo hazina stika za TRA ndani ya mkoa wa Dar es Salaam.
Aidha alisema baada ya siku kumi ofisi yake kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kanda Maalum wataendesha msako wa kuwakamata wote watakaokuwa wamekiuka agizo hilo.
Akiongea na waandishi pamoja na wasanii hao, Mh Makonda aliwaagiza watu wa bodi ya filamu kufanya tadhmini ya haraka kubaini ni maduka mangapi yanayouza mikanda ya filamu jiji Dar es Salaam ndiposa aweze kuchukua hatua inayotakikana.