Hii ndio sababu Harmorapa alitoka kama amevalia nguo za kike (Picha)
Harmorapa ni msanii ambaye hutafuta Kiki kwa kutumia njia yoyote. Kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya Nundu lakini hajaziwacha vituko vyake.
Hivi karibuni aliweka picha kama amevalia nguo za kike akidai kuwa aliiga mwenendo wa Alikiba ambaye kwake ni msanii hatari na wa kuogopwa na wengi. Wikendi iliyopita Kiba alionekana amevaa nguo za wanawake alipokuwa kwenye Lip Sync Battle akiimba wimbo wa Brenda Fassie, Vulindlela.
Harmorapa akizungumza na Kipindi cha E news cha EATV alisema,
“unajua mimi namkubali sana Alikiba, hivyo nilivyoona amefanya kitu kile na mimi nikasema ngoja nifanye kama ‘Cover’ ila sikuvaa gauni la bosi wangu wala sikuvaa gauni. Mimi naona niliva mavazi ya kawaida tu, labda nyinyi ndiyo mnaona gauni lakini kwangu mimi ile ni nguo tu ya kawaida,”