Hii ndio sababu Faiza Alley anasema kuwa wasanii wa Tanzania hawana ubunifu
Faiza Ally ambaye ni mama ya watoto wawili hivi karibuni aliwachana wasanii wa Tanzaniak kwa kudai kuwa hawana ubunifu wowote wa kutafuta Kiki.
Mrembo huyu aliandika haya kupitia Instagram account alisema;
“Nilichogundua sasa hivi kutokana na kipindi ninachosikilizaga redioni ni kwamba wasanii Watanzania hawana akili za ubunifu katika kutafuta kiki, zaidi ya wanaume kutoka na wanawake maarufu na wanawake maarufu zaidi ya kutoka na wanaume maarufu.”
Akamalizia kwa kusema;
“Unapokuwa msanii kiki ni moja ya kazi lakini jaribu kuwa mbunifu kidogo zaidi ya uroda! Sema naomba mnisamehe ni ile uhuru wa kuongea tu sijamlenga mtu lakini najua kuna mstari wa kujifunza”