Hemed PHD Ataja Sababu Za Kukimbia Kuzaa na Mastaa Wenzake
Muigizaji wa Bongo movie Hemed Suleiman ‘PHD’ amefunguka na kutaja sababu za kukimbia kuzaa na Mastaa Wenzake na kuishia kuzaa na wanawake ambao sio maarufu.
Hemed ameweka wazi kuwa amlichagua kuzaa na wanawake ambao sio maarufu kwa sababu hakuona staa wa kike ambaye angeweza kuzaa naye na kisha kuwa mama bora.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Hemed amefunguka na kusema kuwa kwa sasa ana watoto sita ambao amezaa na wanawake tofauti, lakini hakuwahi kuona mwanamke staa mwenye kigezo cha kuzaa naye kwani anapenda wanawake wanaojiheshimu na wenye mapenzi ya kweli.
Ninamshukuru sana Mungu kwa kunijalia watoto sita kwa wanawake ambao hawana umaarufu hata mmoja maana wangekuwa mastaa tungesumbuana sana”.
Hemed ana jumla ya watoto sita na Wanawake tofauti tofauti lakini mtoto wake pekee ambaye amekuwa akimuanika ni wa mwisho ambapo amedai watoto wake wengine Hawaonekani kwa sababu mama zao hawataki.