Haya Ndio Majuto Ya Shamsa Ford Katika Bongo Movie

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford amefunguka na kudai moja ya jambo analijutia maisha yake yote ni kitendo cha kukataa kusoma shule pale alipokuwa mdogo.

Shamsa Ford alifunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amedai kuwa anaumia kila akikumbuka nafasi aliyochezea alipokuwa mdogo kwani Mama yake alimbembeleza sana arudi shule akasome ndio aendelee na kuigiza;

download latest music    

Mama yangu alinikazania sana nisome kwa bidii wakati nipo shule ila nilipomaliza form six nikaona inatosha counter book nikaona zito ila scipt nikaona nyepesi…Natamani ningerudisha siku nyuma ningesoma kwa bidii hata kama ningetaka kuwa muigizaji basi ningekuwa muigizaji wa kimataifa with knowledge. Moja kati ya vitu vikubwa vinavyoturudisha nyuma bongo movie ni elimu. Mtu aliuesoma na asiyesoma ni vitu viwili tofauti sasa sisi wengi wetu hatuna elimu kabisa wengi wao ni darasa la 7,5,2,6 wengine ndio kabisaa alijifunza kusoma na kuandika tu. Nakumbuka mwaka juzi nilimuona msanii wa Nigeria Genevieve Nnaji akiojiwa CNN nikatamani niwe mimi. Wenzetu wamesoma ndio maana wametupita vitu vingi sana”.

Shamsa aliendelea kufunguka mazito kuhusiana na hali halisi ilivyo kwa Bongo movie na filamu zao kwa ujumla;

Yaani huku Bongo movie kumejaa umbea, chuki, roho mbaya, ushirikina. Mtu hata kama hujawahi kumkosea lakini akikaa na watu wanaokuchukia atakusema vibaya, lakini pia ukijitenga useme uishi kivyako utaambiwa unaringa na vikao vya kusengenywa utawekewa juu! Yote hayo ni kwa sababu ya ukosef wa Elimu ndio maana watu wanaweza kupoteza muda kwa vitu vya kijinga. Mwenyezi Mungu nisaidie nimsomeshe mwanangu kwa nguvu zangu zote aje awe mtu wa muhimu kwenye hii dunia na sio Bongo Movie”.

Siku za hivi karibuni tasnia nzima ya bongo mo vie imekuwa ikiandamwa na visa vya kufeli katika kuburudisha huku watu wengi wakithubutu hata kusema kuwa kwa sasa Bongo movie imekufa kabisa.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.