Harmonize Atangaza Kolabo Yake na Burna Boy Toka Nigeria
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Harmonize ameibuka na kudokeza kwa ujio wa kolabo yake na staa wa muziki kutoka Nigeria maarufu kama Burna Boy.
Harmonize ambaye yuko nchini Nigeria kwa sasa ameonekana akiwa na Burnay Boy katika maeneo tofauti tofauti lakini pia akipost moja ya picha aliyopiga na Burna Boy na kuweka wazi kuwa kuna ujio wa kolabo yake mpya na mshindi huyo wa tuzo tatu za Sound city.
Lakini pia Htonize amedokeza ujio wa kolabo hiyo bila kutoa taarifa zaidi Mpaka sasa Harmonize ameshafanya kolabo na wasanii zaidi ya wanne wa Nigeria.