Harmonize Amefunguka Kuhusiana na Ujauzito wa Mpenzi Wake Mzungu
Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka Wasafi Classic Baby (WCB), Harmonize amezidi kusisitiza kuwa mpenzi wake mzungu Sarah ni mjamzito.
Baada ya kutangaza kuwa yeye na mpenzi wake huyo wanatarajia kupata mtoto na kuweka picha mbali mbali mtandaoni zinazomwonyesha mtoto akiwa tumboni (ultrasound), watu wamekuwa wakihoji ile mimba imeenda wapi kwani tumbo lake limezidi kuonekana dogo badala ya kukua kama wanawake wajawazito wengine.
Kwenye mahojiano na Times Fm Lilommy alimuhoji Harmonize juu ya ujauzito huo na haya yalikuwa majibu yake:
Sarah bado ni mjamzito na ninavyoongea na wewe amesafiri maana anajisikia vibaya kutokana na mimba yake amesafiri ameenda Italy nyumbani ila kingine ninachoweza kusema ni kuwa sisi waswahili na wenzetu tunaweza kuwa ni tofauti kidogo na vitu nitofauti yaani ukitumia jicho la kawaida huwezi kujua yaani hapa ninavyo zungumza na wewe anaumwa anaumwa vibaya sana ujauzito unampelekesha”.
Harmonize ameongezea kuwa endapo mtoto wake atazaliwa wa kiume basi atapendelea kumwita ‘Ibrah’.
Baada ya kutangaza kuwa wanategemea kupata mtoto miezi kadhaa iliyopita watu walishangaa kuona Sarah haonyeshi mabadiliko yoyote katika mwili wake ndipo habari za chini chini zilianza kuwa Sarah sio mjamzito bali ni stories waliotengeneza ili kupata kiki na kumuumiza roho mpenzi wake Wa zamani Jacqueline Wolper, habari ambayo Harmonize ameikana mara moja.