Harmonize Ajisalimisha Kituo cha Polisi
Msanii Harmonize ameamua kujisalimisha kituo cha polisi ili kutii amri ya mkuu wa mkoa Paul Makonda aliyoiagiza wiki iliyopita alipokuwa katika mkutano na wasanii nchini.
Harmonize ambae alikuwa akituhumiwa kwa kosa la uvutaji wa madawa ya kulevya yanayosadikika kuwa ni bangi hasa baada ya kusambaa kwa picha katika mitandao ya kijamii akiwa ameweka kitu mdomoni chenye uashiria wa kilevu icho.
Msanii huyo ambae ametua hivi karibuni akitokea nchini Ghana, aliamua kufika kituo kikuu cha polisi jijini na kujisalimisha ili kutii amri hiyo huku ikisemwa kuwa aliweza kushikiriwa zaidi ya saa tano kwa ajili ya mahojiano.