Harmonize Afunguka Baada Ya Raisi Kenyatta Kucheza Nyimbo Yake
Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Harmonize amefunguka Baada ya video kusambaa kwenye Mitandao ya kijamii inayomuonyesha Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta akiwa anacheza wimbo wake.
Video huyo ambayo inekuwa ikitrend kwenye Mitandao ya kijamii imemuonyesha Raisi Kenyatta akicheza Wimbo wa Harmonize ‘Happy birthday’ alipokuwa Anasheherekea Birthday yake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize amemuandikia ujumbe wa shukrani dj wa Kenya ambaye alipiga wimbo huo ambao ulichezwa na Raisi Kenyatta Lakini pia Governor John.
https://www.instagram.com/p/BsV4EfsnBIl/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=rcu8l7jgntg1