Hali ya Ommy Dimpoz Yasemwa Kuwa Mbaya, Arudishwa Hospitali Ujerumani.
Msanii Ommy Dimpoz ambae miezi kadhaa iliyopita aliwahi kuripotiwa kuwa na hali mbaya lakini baadae alikuja kuonekana yuko sawa inasemekana kuwa amerudishwa tena hopsitali hivi karibuni baada ya hali yake kubadilika na kuwa kama ilivyokuwa awali.
Msanii huyo ambae hali yake inasababishwa na hali aliyokuwa nayo mwanzoni baada ya kufanyiwa upasuaji wa koo na alitakiwa kurudi nchini Afrika ya Kusini kwa ajili ya vipimo na kukutwa kuwa bado yuko na shida hivyo anapaswa kurusi hospitali nchini Ujerumani.
Mpaka sasa inasemekana kuwa msanii huyo yuko nchini Ujerumani kwa ajili ya kukutana na daktari wake ili kurekebisha baadhi ya sehemu ambazo zinaonekana zitaleta shida.