Hali ya Jini Kabula Yaimarika,Amshukuru Esha Buheti
Msanii wabongo movies Jini Kabula amekairi kuwa kwa sasa hali yake ya kiafya imehimarika sana na yupo mwanza kwa kaka yake ambapo bado anajitazamia hali yake. Msanii huyo ambae alikuwa kama mtu aaliyeugua uchizi baaada ya kusemekana ni athari za matumizi ya madawa ya kulevya alipelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi .
Hata hivyo Jini Kabula amekuwa akilalamika kwa wale ambao wamesambaza taarifa kuwa yeye ni muathirika wa Ukimwi, na kusema kuwa watu hao hawamtakii mema na habari hizo hazina ukweli wowote zaidi ya kuwa anachukiwa na baadhi ya watu.
Jini Kabula anamshukuru Esha Buheti kwa wema alimfanyia kipindi chote alichokuwa akiumwa na kwa msaada mkubwa aliompa huku akisema kuwa kipindi anaumwa kuna baadhi ya watu wake wa karibu walikuwa wamemtenga kabisa na hawakutaka hata kujua hali yake.
Ni kweli kuna watu walikuwa mbali na mimikabisa, lakini ni kawaidasana hasa kwa ugonjwa kama niliougua mimi nivigumu sana watu kutaka kuwa karibu na mimi kwakweli lakinibado nina washukuru sana baadhi ya wasanii wachache waliopambana sana katika kuokoa maisha yangu hasa dada yangu Esha Buheti , Mungu ambariki sana na hakika maisha yake yamebalikiwa sana, ni mwanamke mwenye roho ya utu na uungwana wa kupitiliza.
Hata hivyo Jini Kabula anasema kuwa kwa sasa ameshaachana na hanasa zote na amekuwa mtu wa Mungu kwa sababu matatizo yaliyompata ni makubwa na atakuwa mjinga kama atarudi kule kwasababu aliteseka sana.
Wasanii wengi wamekuwa wakilalalmika kuwa wanapopata matatizo ni wasanii wenzao wachache wanaosimama nao na kuwashika mkono katika matatizo hayo, wengi uendelea na shughuli zao na kusahahu kuwa mtu huyo aliepata matatizo walikuwanae wote katika starehe kipindi hayuko na matatizo.