Hali ya Hawa wa Nitarejea ni Mbaya Huko Muhimbili

Kama tunakumbuka Diamond alishawahi kuimba wimbo wa nitarejea na kumshirikisha dada mmoja aliyekuwa na sauti nzuri ya kumtoa nyoka pangoni.Mwanadada huyo aliyekuwa akijulikana kwa jina la Hawa alikuja kupotea ghafla katika tasnia pamoja na kwamba hakukaa kwa muda mrefu katika game.

Mwanadada huyo kwa sasa yuko hoi kitandani katika hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na ugonjwa wa ini unaomsumbua kwa muda mrefu sasa.

download latest music    

Moja ya wamiliki wa kituo cha kusaidia watumiaji wa madawa ya kulevya ambako Hawa alikuwa akitibiwa,  Pili Misana alisema kuwa kwa muda mrefu sasa hawa amekuwa na tatizo la ini ambalo kwa kiasi kikubwa limesababishwa na utumiaji wa muda mrefu wa madawa ya kulevya na unywaji wa pombe kali.hata hivyo pili missana anasema kuwa hali ya hawa ilianza kuimarika kwa sababu alikuwa tayari alishakubali kutoka katika matumizi hayo lakini kumbe alikuwa tayari ameshaanza kuathirika ini.

unajua hali ya hawa ilikuwa tayari ilishaanza kutengemeaa,lakini kumbe alikuwa tayari ameshapata tatioz la ini muda mrefu. kutokana na unywaji wa pombe kalikwa sasa hivi hali yake sio nzuri na anaendelea na  matibabu katika hospitali ya muhimbili.-Alisema Pili Misana.

Ikumbukwe kuwa Hawa alishawahi kuripotiwa na kipindi cha shilawadu siku za nyuma kuwa ameathirika sana na utumiaji wa madawa ya kulevya  na wazazi wake kuomba asaidiwe ili arudi katika hali yae ya kawaida.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.