Godzillah Afungukia Tetesi Za Kuwa Chapombe
Msanii wa muziki wa Hip hop nchini Golden Jacob Mbunda ‘King zilla’ au ‘Godzilla’ au ‘Zilla’ ameibuka na kukana tetesi ambazo zimekuwa zikidai kuwa amepotea kwenye gemu kisa kunywa pombe.
Kwa muda sasa kumekuwa na tetesi kuwa Zilla amepotea kwenye gemu na mambo mengi yamekuwa yakizungumzwa juu yake. Pombe imekuwa ikitajwa kuwa ni chanzo cha yeye kupotea.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Amani, Godzilla alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo alikana mara moja na kuweka wazi kuwa hayo ni maneno tu ya wanadamu:
Huwezi kumzuia mtu mwenye mdomo kuongea kwa hiyo ndiyo hulka ambayo tunayo especially Watanzania. Kwa watu ambao wanamjua Zilla, ni mtu ambaye anapenda sana kuishi maisha ya kawaida, nakaa kitaa, napiga stori mbili-tatu na washkaji kwa sababu ndiyo wanasapoti kazi zangu, siwezi kuwavimbia, lazima nitafute muda wa kuongea nao na kupata mawazo kutoka kwao. Kuhusu pombe, kila mtu na starehe yake, wengine tukipata mbili-tatu zinatupa vibe la kutoa vitu vizuri, lakini sinywi kupitiliza kama wanavyosema”.
Lakini Godzilla alifungukia ukimya Wake kwenye gemu kwa muda mrefu na kudai yupo kimya akijiandaa kwa ajili ya kazi mpya:
Nipo kimya kwa muda kwa sababu naandaa albam yangu mpya ambayo bado mpaka sasa sijapanga lini nitaitoa inayokwenda kwa jina la 55555. Imebeba nyimbo nyingi nzuri, watu watainjoi muziki mzuri kwa sababu wanajuaga ninachokifanya ninapokuwa nimetulia.