Gigy Money na Mo J Mapenzi Moto Moto Tena
Video vixen na msanii wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money ameonekana tena na baba wa Mtoto Wake Mtangazaji wa Choice Fm Mo J siku chache Baada ya kuachana.
Wiki iliyopita habari iliyotrend kwenye Mitandao ya kijamii ni kitendo cha Mo J ambaye alikuwa kwenye mahusiano Gigy Money kudaiwa kumtongoza mke mtarajiwa wa Mc Pilipili na kumwagwa chini.
Kupitia katika kipindi cha Shilawadu Gigy Money alionekana akitoleana Povu zito na Mo J na hata kumtukana kupindukia na kutangaza kuwa amemuacha na yuko single.
Lakini inaonekana wawili hao hawajaachana kwa muda mrefu kwani siku ya Leo kuna video clip inawaonyesha wawili hao wakiwa wamerudiana na wanaonekana wakiwa pamoja.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Gigy Money anekiri kurudiana na baba Watoto Wake na kudai kuwa anahisi kuwa amelogwa na Mpenzi Wake huyo.
Yaani mimi najua huyu kaka kaniloga tu jamani na sitaki kuelewa”.