Gigy Money Akiri Kuacha Utoto,Ajiandaa Kuwa Mama Bora.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchi Gify Stanford almaarufu kama Gigy Money amefunguka na kusema kuwa anataka kujitahidi kuwa mama bora kwa mtoto anaetarajia kumpokea hivi karibuni hivyo tabia za kitoto zote anaachana nazo kwa sababu huko siko aliko sasa.
Gigy Money amabe kwa sasa ni mjamzito na anatarajia kujifungua siku yoyote amesema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na Showbitz extra na kusema kuwa hata yeye anajiona kuwa amebadilika na hii ni kutokana na ukweli kwamba unakuwa mjamzito hatua inayofuata ni kuwa mama na sio kurudi nyuma tena hivyo ili kuwa mama bora ni lazima kukubali hali hiyo na kuachana na mambo ya nyuma.
nimekuwa kwakweli unajua huu ujauzito umenipa funzo la maisha, na sasa naenda kuwa mama na hili niwe mama bora basi ni lazima na kila kitu sio niendelee na maisha yale ya kitoto niliyokuwa nikiishii zamani.- Alifunguka Gigy Money
Wikiendi iliyopita Gigy Money alifanya baby shower, sherehe ambayo ufanyiwa mama mjamzito kwa ajili ya kumpa zawadi na kumuandaa kwa ajili ya kujifungua kwake.