Gigy Money Adai Anamuacha Mtoto Wake Ili Kusaka Pesa
Video vixen na msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amekiri kuwa anamuacha mtoto wake nyumbani mara nyingi lakini amesisitiza ni katika harakati za kusaka pesa.
Gigy Money amekuwa akikosolewa sana kutokana na kuonekana akiwa katika kumbi mbali mbali za starehe wakati mtoto wake akiwa na wiki kadhaa tangu azaliwe.
Gigy amefunguka na kujitetea kuwa sababu pekee ambayo inamfanya asafiri na kumuacha mtoto wake nyumbani ni kusaka pesa kwa ajili ya malezi ya mtoto wake.
Kwenye mahojiano na Kipindi cha XXL cha Clouds Fm amesema ni vigumu yeye kulala nyumbani wakati hana fedha:
Nilienda Nairobi nikakaa mwezi mzima na nilimuacha mtoto na mama yangu, hakuna mtu anaweza kuacha dola 4,000 (sawa Tsh. Milioni 9) kirahisi“.
Gigy Money amesisitiza kuwa ingawa anapenda kukaa nyumbani na mtoto wake Myra lakini amesema hawezi kufanya hivyo kwani Familia yake inamtegemea.