Gigy Akiri Kuishi Kwa Kudanga

Mwanadada asiyeisha vituko katika mitandao ya kijamii Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amefunguka na kusema kuwa jinsi anavyoishi yeye ni tofauti kabisa na vile watu wanavyomchukulia kwa sababu watu wanahisi yeye ana ela sana lakini kumbe maisha yake ni magumu tu na anaishi kwa kudanga  na kufanya badhi ya madili ya mtaani.

Gigy anasema kuwa kwa kifupi jina lake limekaa kipesa pesa ndo maana wengi  wanafikiria kuwa yeye anapesa nyingi sana lakini ukweli ni kwamba wala hayuko hivyo kabisa zaidi ya kupigika kimaisha. Gigy anasema kuwa anachoshangaa ni kwanini watu wamekuwa wakivutiwa sana na jina lake hili.

download latest music    

Jina langu tamu sana,maana yake hata jinsi linavyo-sound  ni jina moja zuri ambalo limekaa kipesa pesa tuu, lakini ajabu pamoja na uzuri wa jina langu hilo  maisha yangu mimi mwenyewe hayafanani kabisa na jina langu, naishi kwa kudanga tu na kufanya madili ya hapa na pale

Gigy Money  alishawahi kukiri kipindi cha nyuma katika chombo kimoja cha habari kuwa alikuwa akifanya kazi ya kuuza mili kwa wattu mbalimbali ikiwepo vigogo ili kuweza kujimudu kimaisha.

Ukiachana na kuuza sura katika video mbalimbali lakini pia Gigy Money kwa sasa amejiingiza katika kazi ya sanaa na pia ni mtangazaji wa kipindi fulani katika radio moja jijini, mashabiki wamekuwa wakishangazwa na mwanadada huyo ambae amekuwa na vipaji tofauti tofauti lakini bado anakiri kuwa yeye ni mdangaji.

Haitakuwa kauli ya  kwanza kwa Gigy Money kuongelea maisha yake na biashara hiyo ya udangajiLlakini pia hii ni moja ya tabia ya wasichana wengi Tanzania wanojifanya kujiingiza katika muziki huku wakitumua sanaa kama mwamvuli  wa kuwafunika huku nyuma ya pazia wakufanya mambo mabaya kama hayo ya udangaji.

Lakini kwa kuwa Gigy Money amekuwa ni mmoja wa watu waliopewa vipaji vingi ikiwemo hiki cha muziki nadhanisasa anapaswa kuacha kutaka kuishi maisha yasiyo ya kiwango chake na kujikitazaidi katika kazi halali itakayompa ela

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.