Gari la Wastara Lakamatwa Bandarini, Aiomba Msaada Serikali
Baada ya mwanadada wastara kulalamika siku chache zilizopita kuhusu swala la kuibiwa na majambazi vitu vyake vya kufanyia kazi hivi karibuni , ameibuka tena na kulilia swala la gari lake kutoka nje ya nchi kukwama bandarini huku sababu ikiwa ni Pesa.
Wastara anasema kuwa gari hilo alilopewa msaada na marafiki zake kutoka nje ya nchi limefika tanzania siku nyingi lakini amekuwa akishindwa kulitoa bandarini hapo kwa sababu ya fedha.
Wastara anasema kuwa ameshakwenda mpaka kwa waziri kufatilia swala hilo lakini bado haoni kama kuna msaada wowowte anaweza kupatiwa kwa watu aliowafikia zaidi ya maumivu,
Wastara anasema kuwa watu hao waliamau kumpa gari hilo baada ya kumuona akiwa anaangaika sana na matatizpo yake ya mguu hivyo kuamua kumrahisishia kwa kumpa usafiri ili aweze kufanya mambo mengine kwa urahisi zaidi,
Wastara anasema kuwa watu wasihangae kama atakufa ghafla kwa sababu amekuwa mtu wa mawazo sana muda owte kutokana na maisha anayoishi ya kuwa na mawazo muda wote.