Gabo afunguka kuhusu uhusiano wake na Wema Sepetu
Baada ya Wema Sepetu kuachia picha za kimapenzi akiwa na Gabo Zigamba, wengi hivi sasa wanaamini kuwa wawili hao wanatoka kimapenzi kitu ambacho Gabo amekana.
Gabo Zigamba pia amekuwa akizipata habari ambazo zinadai kuwa hivi sasa anamchumbia wema lakini kwa mara ya kwanza ameweza kufunguka kuhusu uhusiano wao. Muigizaji huyu amefunguka kwa kusema kuwa picha zake na Wema Sepetu ni za kikazi wala sio kimapenzi.
Alisema kuwa picha hizi zinaonekana kuwa zakimahaba kwa sababu hivi karibuni wanapanga kuachia movie itwayo Heaventsent ambayo inazungumzia mapenzi. Alisema,
“Movie tunayoifanya na Wema iko very tomantic ndio maana hata picha zenyewe lazima ziwe hivo sasa watanzania naona wao washarasimisha kwamba kuna kitu kinaendelea kumbe hakuna pale tupo kazini na niwaahidi mashabiki zangu naanda kitu kikali sana mara mbili za jinsi wanavyonifahamu.”
Muigizaji huyu amesema haya wiki kadhaa baada ya Wema Sepetu pia kukana mahusiano yake na Gabo.