Florah Mbasha Amefunguka Kuhusu Utata Unaoizunguka Ndoa Yake

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili Florah Mbasha au kwa sasa anajulikana zaidi kama Madam Florah amefunguka na kuongelea ndoa yake na kuondoa utata uliokuwa unaizunguka.

Mwaka Jana 2017, Florah alitangaza kuwa anaolewa na mume wake David Kusekwa baada ya kutengana na mume wake wa miaka mingi Emanuel Mbasha. Pamoja na kwamba harusi ya Florah na David ilikuwa ya wazi kwenye mitandao ya kijamii lakini ndoa yake imekuwa ya siri.

download latest music    

Lakini tangu ndoa yao imefungwa wawili hao wamekuwa kimya sana kwenye mitandao ya kijamii kiasi ya kwamba kumekuwa na tetesi kwenye mitandao ya kijamii wawili hao hawapo pamoja.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5 Florah amefunguka na kusema kuwa yeye na mume wake Daudi Kusekwa wako pamoja na wako vizuri na hajawahi kujutia hata mara moja kuolewa na mume wake.

Madam Flrah amezidi kufunguka haya kuhusu ndoa yake:

Mume wangu ni gentleman anajiheshimu ana hofu ya Mungu na ana Upendo wa kweli kwangu, to be honest nina bahati kubwa na sijutiii kuwa mke wake wa ndoa, Namshukuru sana Mungu kwa ajili ya Daudi my husband. When it comes to mume wangu sisikii wala siambiwi mana tulipendana wawili watatu wanatokea wapi? Mapenzi ni ya wawili so ni vyema kuziba masikio na kufanya mambo yako maana maneno ya watu hayajengi bali huishia kubomoa”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.