Florah Afunguka Baada Ya H.Baba Kukiri Kumiss Uwoya
Msanii wa filamu za Bongo movie, Florah Mvungj amefunguka Baada ya mume Wake ambaye ni Msanii wa Bongo fleva H. Baba kukiri kumiss Ex Wake Irene Uwoya.
Siku chache zilizopita H-Baba kupitia ukurasa wake wa Instagram aliweka picha ya Irene Uwoya kisha kuandika kuwa amemmisi, jambo lililowashangaza wengi kwani siku za nyuma kidogo aliwahi kumponda na kusema haoni ndani kwa mke Wake Flora.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Florah Mvungi amedai haoni tatizo kwa Mume Wake kumkumbuka Aliyekuwa Mpenzi Wake isitoshe amedai yeye hana wivu.
Watu wanakuza mambo sana, mbona ni hali ya kawaida sana, ni kumbukumbu tu ambazo mtu zinamrudia, anafanya anachojisikia, ameona ni vyema kushea kumbukumbu zake na watu kwenye mitandao, sijaona shida yoyote na wala sijahisi wivu“.