Fid Q Ampa Shavu Msanii wa Taarab
Msanii wa muziki wa Hip hop nchini Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q amempa Shavu Msanii maarufu wa Taarabu nchini Isha Mashauzi katika kazi yake mpya.
Wimbo mpya wa Fid Q unaenda kwa jina la ‘Bam Bam’ iliyowakutanisha Isha Mashauzi, Rich Mavoko na Big Jahman huku Wimbo huo ukimya umetengenezwa na Marco Chali toka Mj Records.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Clouds Fm, Fid Q amefunguka na kusema kuwa ameamua kumshirikisha Isha Mashauzi ambaye amezoeleka kuimba muziki wa Taarabu kwa sababu ya uwezo Wake wa kuimba kwa style nyingi.
Yaani kilichotokea Mpaka nikamfikiria nilikutana naye sehemu anaimba covers na nyimbo nyingine nyingine nikasema HA! Mbona mimi nilijua unaimba taarabu tu wewe, akasema hapana mimi naimba muziki aina tofauti tofauti.
Kwaiyo nilipokuwa studio nilisema nahitaji mtu ambaye ana tabia ya kupita na mistari yangu ndio ilifanya apate attention yangu”.