Feza:Nilisema Sitaki Mwanaume Mwenye Ngumi

Mwanadada anaetamba kwa sasa na kibao chake cha simple Feza Kessy amefunguka magumu aliyowahi kuyapitia katika mahusiano yake yaliyopita na kusema kuwa amekuwa akikaa katika mahusiano kwa muda mrefu lakini mwisho wa siki watu wanamuumiza kabisa.

Feza Kessy amesema mahusiano yake ya mwisho yalikufa mwaka jana na hakutaka kuyaweka wazi kwa sababu kipindi yuko na Onel kutoka Big Brother alikuwa na mahusiano ya wazi lakini hayakudumu hivyo aliona yanayofuata ni lazima yawe kimya.

download latest music    

Hata hivyo Feza ameelezea kuwa sababu kubwa ya yeye kuachana na Onel ilikuwa ni baada ya mwanaume huyo kumpeleka kwao na kumpiga sana kichapo cha mbwa mwizi kisa wivu wa mapenzi.

Sio kwamba alikuwa ananipiga sana kila siku , hapana lakini kuna siku aliniwashaaa,alikuwa na wivu tangu tupo kwenye jumba la big brother,na kwa uelewa wangu mtu wmenye mkono wa kupiga ni vigumu sana kuacha.

Kuna namna mtu anaweza kukupiga na ukajua kabisa kuwa amekupiga kwa sabab umemkwaza hasa lakini yeye alinipiga vibaya, mpaka nikaita polisikwa kosa gani  labda.Niliondoka na wala sikutaka kurudi tena kwa sababu nilikuwa kwao, wala sikuwa nyumbani kwetu ,sikuwa na mtu wa kunitetea au kuongea nae.nikaja nikashare kuwa no more Oneza.Na nikasema kabisa on Twitter kuwa sitaki mwanaume mwenye ngumi.

Feza Kessy aliingia katika jumba la mashindano ya Big Brother mwaka 2013 akiwakilisha tanzania, ambapo akiwa kule akijiingiza katika mapenzi na moja  ya washiriki kutoka Botswana na kufikia hatua ya kufatana  na kutambulisha kwa wazazi.Lakini baadae mahusiano hayo yalikuja kufa na Feza FKessy hakutaka kuweka wazi sababu ya kuachana kwao kwa kipindi kirefu.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.