Faiza Ally: Tanzania nzima na East Africa tunatakiwa tumpenda Diamond sana
Faiza Ally amedai kuwa ni sharti Tanzania na Afrika Mashariki nzima kumpenda Diamond. Mrembo huyo aliandika ujumbe wake kwenye mtandao wa Instagram.
Ally alimpigia kifua Diamond kwa kusema kuwa muziki wa Tanzania haukua na ushindani kabla ya Diamond kuingia kwenye game.
“Hivi hamjawaji kujiuliza kwamba toka zamani kabla ya Diamond kulikua na mziki mzuri lkn hakujawahi kuwa na ushindani kama changamoto alio leta Diamond kwenye game. Hivi mnajua kwamba Tanzania nzima na East Africa tunatakiwa tumpenda Diamond sana ???? Hivi hamjawaji kujiuliza kwamba toka zamani kabla ya Diamond kulikua na mziki mzuri lkn hakujawahi kuwa na ushindani kama changamoto alio leta Diamond kwenye game , sasa nasema hivi mziki mzuri peke yake hautoshi na akili kubwa inahusika , unapo kuwa huna akili ktk unalo lifanya ni sawa na mwanamke mzuri hlf hajielewi…. Leo hii kwa u star wenye akili alio uleta Naseeb wazazi wengi wanaona fursa ya mziki kupitia Diamond tofauti na miaka ya zamani, mziki ulikua unaonekana kama sio kazi lkn Leo mziki unaendesha familia nyingi, hata mm ningependa mwanangu awe mwanamziki mwenye mafanikio kama Diamond , sasa nasema hivi ku mpenda Diamond ni amri sio ombi,” aliandika Faiza Ally.
Aliandelea kwa kusema kuwa Diamond ni kama Obama:
” Diamond ni kama Obama marekani kwa watu weusi , yeye alionyesha kuwa mtu mweusi ana uwezo kwenye siasa na Diamond tanzania kaonyesha mziki unalipa na msisahau katoa vijana wengi na bado wengine wamepata ajira kupitia yeye na naona watapata wengi zaidi ! Sasa nakuomba D ufungue music school basi tuwalete watoto wetu na wenyewe wapate mkwanja kama wako maana shule sio maisha pekee mention town na vipaji navyo ni sehemu ya mafanikio ktk maisha a special kwa maisha tunayo elekea , mm nakupendaga sana na zaidi ni jitihada zako kwenye kazi ! Keep it up dogo ? #ZILIPENDWA”