Faiza Ally: Diamond Bado Kijana Mdogo Hayupo Tayari Kuoa
Tangu jana kumekuwa na tetesi kwenye mitandao ya kijamii ya kuwa Zari na Diamond wameachana habari hizo zilisababishwa na ujumbe alioweka Zari na kitendo chake cha kufuta picha zote za Diamond kwenye ukurasa wake wa Instagram, hii imetokea siku chache tu baada ya Zari kumsamehe Diamond baada ya kuzaa na Hamisa Mobetto ambapo watu waliamini wamesameheana na yameisha.
Muigizaji na mwanamitindo Faiza Ally amefunguka na kudai kuwa hadhani kuwa Diamond yupo tayari kuoa na kutulia chini na familia kwasababu ya umri wake kuwa bado mdogo.
Kwa kupitia ukurasa wake wa Instagram Faiza ameandika yafuatayo;
“Diamond kijana mdogo sana anahitaji kuhave fun na watoto wenzie na sisi wadada tuangalie watu wakutoka nao…..nenda baba have fun ndo usettle down….jiachie uwe huru ikibidi uwe na mahusiano bado hujaiona dunia hata nusu wewe ni star, hela ipo there is a lot to see. Naongea kwa roho nyeupe sina chuki na Zari au kwa yoyote nimezurura sana duniani kabla ya kuzaa na kutulia jiachie bwana life is today”.
Aliandika Faiza ambaye ameshawahi kuweka wazi kuwa yeye ni shabiki wa Zari.