Faiza Aja na Kampeni ya Single Mothers ,Ni Kwa Wamama Wenye Majukumu ya Kulea Watoto Peke Yao
Mwanadada Faiza Ally ambae pia ni mfanya baishara maarufu bongo amekuja na kampeni ya single mothers itakayowakutanisha wanamama wanaolea watoto wakiwa peke yao bila kuwa na baba zao.faiz ameamua kufnaya hivyo ili kukutana na wanawake wanaobeba majukumu ya familia wakiwa kama mama na pia wakishika nafasi ya baba ambao wanapatikana wengi sana katika jamii zetu.
Akiwa kama mmoja wa wanawake hao kutokana na kulea mtoto wake wa kike peke yake kwa muda mrefu huku ikisemekana kuwa baba wa mtoto wake muda mwingi alikuwa akikataa kutoa matunzo kwa mtoto wake anaalika wanawake wengine kuja katika siku hiyo ya kukutana kwao ambapo itafanyika april 7 mwaka huu na kuongea matatizo yanayowakabili.