Esther Kiama Atamani Nafasi Ya Jokate
Muigizaji wa Bongo movie Ester Kiama amefunguka na kuweka wazi kuwa ametokea sana kumtamania mrembo Jokate Mwegelo ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Ester alidai kuwa, kwa sasa Jokate amekuwa ‘role model’ wake na anaamini siku moja atakuwa kama yeye.
Unajua nimejikuta natamani kuwamkuu wa wilaya flani hivi ingawa najua siyo mchezo kama watu wanavyofikiria. Kiukweli Jokate ndiyo amenifanya nitamani hivyo, navutiwa na utendaji kazi wake lakini pia anavyonyuka zile suti. Na mimi nimeshaanza kumuiga katika uvaaji”.
Miezi michache iliyopita Mrembo Jokate Mwegelo aliteuliwa na Raisi Magufuli na kuwa mkuu wa Wilaya ya Kisarawe na mara moja mrembo huyo ameonekana kufanya vizuri sana katika nafasi yake na kuwatumikia vyema wananchi.