Esther Kiama Agoma Kuanika Mipango Yake Kuhofia Wanga
Muigizaji wa Filamu za Bongo movie Esther Kiama ameibuka na kudai anahofia kuanika mipango yake ya mwaka 2019 kwa kuhofia wanga wataweza kumkwamisha.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Ester alisema mwaka ujao anatarajia kufanya kitu kikubwa, lakini hawezi kukitaja kwa kuwa wanga watampiga juju na kushindwa kufikia malengo yake.
Nimejifunza kwamba kwa mwaka huo unaoanza ni vyema nikafanya vitu kimyakimya hadi vikamilike maana nikianza kutangaza, wanga wasiopenda maendeleo yangu, wataya-katisha fasta na kujikuta nashindwa kusonga mbele”.
Esther Kiama ameigiza sinema nyingi za Bongo movie lakini filamu moja ambayo imempa umaarufu zaidi ni ‘Muhanga’.