Enock Bella :Upendo wa Ya Moto Bado Uko Pale Pale
Moja ya wasanii ambao waliokuwa wanaunda kundi la Ya moto Band Enock Bella amefunguka na kusema kuwa watu wengiwameku wakisema kuwa kundi la ya moto band limekuwa halina mawasiliano na wamekuwa katika mgogoro tangu wametengana na kwamba hawataweza kufanya chochote pamoja lakini maneno hayo si ya kweli hata kidogo.
Enock Bella amesema hayo alipouwa akiongea na Times Fm katika kipindi cha The Playlist na kuongezea kuwa watu watakuja kushangaa sana pale ambapo wasanii hao watakuja kufanya kazi tena pamoja hata kama kila mtu yuko chini ya uongozi wake.
Itafika sehemu tutachukua nyimbo za ya moto band na kuzipeleka tena kwa mashabiki wetu,usishangae kusikia kuna ngoma yangu na Aslay, au ukasikia ngoma yangu na beka au moja kati ya hao na Maromboso.bado upendo wetu uko palepale.
Baada ya Ya Moto Band kusambaratika katika umoja wa band yao wasanii hao walianza kufanya kazi kila mmoja chini ya uongozi wao huku Aslaya akiwa wa kwanza kutoa nyimbo zake na zimekuwa nyingi kuwazidi wote , huku Maromboso nae akiwa amechukuliwa na uongozi mpya wa wasafi na kwa sasa ameanza kuachia ngoma zake.