Enock Bella Kulikwaa Dili Kubwa Burundi.
Msanii wa muziki wa bongo fleva ambae hivi sasa anatamba na kibao chake kikubwa kama Sauda na bado kidogo amefanikiwa kulamba dili kuwa na moja ya kampuni kubwa nchini burundi kwa kutaka kusimamia kazi zake za kimuziki.
Enock bella ambae tangu kufa kwa band ya ya moto amekuwa akifanya kazi mwenyewe huku akiwa ni moja ya wasanii waliokuwa wakisema kila siku kuwa wanatamani sana uongozi wa Ya Moto uendele kuwasimamia .
Wakati wa kusainishana kwa mkataba huo kati ayke na kampuni hiyo inayojulikana kama chakor music group, meneja wa kampuni hiyo amesema kuwa lengo lao kubwa ni kutaka ku-push muziki wa tanzania kufanya vizuri na kuendelea kukua .
Tumeingia Tanzania kusaka vipaji vya muziki na tumekuja tukaona kuwa Enock Bella anauwezo mkubwa na kazi zake tumezifuatilia tumeziona ana sauti nzuri, anajua kuimba na ana muziki mzuri.Tunaamini kuwa tutafika nae mbali kwa sababu ana radha nzuri na tofauti ya muziki wake katika kuimba na kutunga pia.
Kwa upande wa Enock pia amefunguka na kusema kuwa ni faraja kubwa tena hasa baada ya kuvunjika kwa kundi la ya moto.
Sikujua kama kazi ninayoyafanya inapenya hadi mbali kiasi hicho.namshukuru mungu kwa chakor kuniona na pia kwa kupata management yangu mpya.naamini kuwa sasa muziki wangu utafika mbali zaidi na nitafanya vizuri kulio hata vile nilivyokuwa nikifanya mwanzo