Ebitoke Ajibu Tetesi za Kujichubua
Siku chache baada ya mwanadada Ebitoke ku-break the internet baada ya kuweka picha katika ukurasa wake akiwa beach, mwanadada huyo aliaandamwa sana kwanza kutokana na kuzoeleka kwake na muonekano wake hakuwahi kuonekana akivaa nguo za wazi kiais icho.
Hata hivyo, mwanadada huyo alisemwa pia kuwa picha hiyo imeonuesha kwa sasa jisni mwanadada huyo alivyojichubua na ngozi yake imebadilika sana sio kama Ebitoke yule aliyekuwa zamani.
Akiandika katika ukurasa wake wa instagram, ebitoke amesema kuwa watu hawapaswi kuamini sana kila wanachokiona katika mitandao ya kijamii kwa sababu vitu vingine vimekuwa editing na havina ukweli wowote.
Katika ukurasa wake Ebitoke aliandika “haya lo nimewawekea rangi yangu ya ukweli, zingine zote fake am still black.mpunguze kusema kuwa najichubua tatizo mnaapenda kuamini mitandaoni maediting na usiamini kila unachokiamini.”