Ebitoke Adai Management Haijawahi Kumpa Gari Wala Nyumba Kama Ilivyodai
Msanii maarufu wa vichekesho katika mitandao ya Kijamii Ebitoke amefunguka na kuweka wazi kuwa hajawahi kupewa gari wala nyumba kama ilivyowahi kusikika katika siku za nyuma.
Siku chache zilizopita Ebitoke alitangaza kuachana Rasmi na Management yake ya Timamu ambayo ilikuwa inamsimamia tangu alipoanza kufanya sanaa yake.
Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Ebitoke amekana taarifa za yeye kupewa gari na Nyumba na Timamu kama ilivyowahi kusikika siku za nyuma:
Hivyo vitu nimekuwa nikiilizwawsana naomba tu leo niseme ukweli siku ya leo, Mimi sijawahi kupewa gari yaani sina gari wala sijapewa nyumba ila nina kiwanja Changu kipo nyumbani karibia namaliza kujenga”.
Ebitoke ameweka wazi kuwa kwa sasa yuko mwenyewe kama yeye tangu alipojiengua Kwenye kundi hilo la Timamu.