Dudubaya Amtolea Povu Zito Nay Wa Mitego
Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva nchini Godfrey Tumaini maarufu kama Dudubaya ameibuka na kumtolea Povu zito msanii mwenzake Nay wa Mitego.
Dudubaya amerudi kwa kasi ya ajabu kwenye headlines Baada ya kuwa kimya kwa miaka mingi tangu alipoacha kufanya muziki miaka michache iliyopita lakini tangu arudi kwenye ramani na Wasafi Festival Dudubaya amekuwa akitrend Sana.
Dudubaya ameibuka na kumjia juu msanii mwenzake Nay wa Mitego ambaye Hivi karibuni ametajwa kuwa na bifu na msanii mwenzake Diamond Platnumz ambaye hapo nyuma alikuwa mshkaji Wake pia.
Baada ya Nay wa Mitego kuwaponda wasanii wa Wasafi, Dudubaya amemtolea Povu hilo Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari:
Unamuona msanii kama Nay wa Mitego anasema wit wasanii wa Wasafi hawana amsha amsha hivi ana akili timamu? Nay wa Mitego alitumwa na Clouds kuandika wimbo wamepanda wameshuka kunitukana mimi na P-funk Anawatukana malegendary waliozaa Bongo fleva”.
Lakini pia Dudubaya aliendelea kumtolea maneno Nay wa Mitego ikiwemo kudai kuwa amebuma na muziki wake umebuma:
Nilimwambia mdogo wangu Nay wa mitego siku zako zinakuja na chamoto utakiona, cha moto anakiona sasa amegombana na T. touch na sasa kila akitoa nyimbo inabuma na wale waliomwambia tunga wimbo uwaponde wakina Dudubaya siku hizi hawapigi nyimbo zake”.