Dudu Baya Amfananisha Mr.Nice na Dk Shika.
Wasanii wakongwe katika muziki Mr nice na Dudu Baya wamejikuta wakiingia tena katika headlines baada ya kuanza kutambia kuhusu ujuzi walionao kimziki kutokana na wao wote kuwa wakongwe.Kwa upande wa Dudu Baya nasema kuwa anashangazwa na kitendo cha Mr.Nice kumwambia kuwa anaweza kumsaidia akainuka kimuziki wakati yeye ndio yuko hoi taabaan hajiwezi anahitaji msaada mkubwa.
Akiongea na eNews Dudu Baya anasema kuwa Mr.Nice kwa sasa ana hali tete sana na anahitaji msaada mkubwa ili kuweka kukaa sawa na aache kuwa na tabia ya kutangaza utajiri wa ndoto na fake kama vile anavyofanya Dk.Shika.
Kauli zake za kuchekesha, ni mgonjwa na ni mahututi kabisa taanbani,hawezi kumsaidia mtu mwenye afya njema hata mara moja.Kwanza hata kauli zake mimi namjua vizuri, hali ya Mr.Nice ni mbaya kiafya hadi kiuchumi.ameathirika kisaikolojia na ndio maana anaota yake ya umaarufu ya kipindi kile, mpunga aliopiga iksha ukayeyuka , kuropoka kutaka kunisaidia mimi ni sawa na Dk.Shika ambae anaota ana hela iko Urusi.
Dudu Baya anasema kuwa hata hivyo Mr.nice sio msanii mzuri kama watu wanavyofikiria kwa sababu hana uwezo wa kuandika mashairi vizuri zaidi ya kuandika nyimbo zinazoimbwa mashuleni na watoto.
Wakongwe hao wanahitaji kukaa pamoja na kusaidia wasanii wanaochipukia kwa kuwafundisha na kuwapa uzoefu badala ya kukaa na kuanza kurushiana maneno katika mitandao.Wanatakiwa kuchukua mfano wa watu kama DullY Sykes, au Lady Jay Dee.