Dr.Cheni Awashangaa Wanaosema Hukumu Ya Lulu Haitoshi
Msanii mkonwe wa filamu za bongo ambae pia kwa muda wote amekuwa mlezi wa msanii lulu michael na amekuwa bega kwa bega na lulu pamoja na familia yake katika kufatilia kesi ya msanii huyo Dr.Cheni amefunguka na kuwashangaa wanaosema kuwa hukuma aliyopewa lulu ilikuwa haitoshi na haikulingana na kile alichokifanya.
Dr.Cheni amefunguka hayo baada ya kuona watu wamekuwa wakiongea katika mitandao ya kijamii na kusema kuwa hukumu ya msanii huyo haiendani na mauaji aliyoyafanya na wengine wakifikia hadi hatua ya kupendekeza kuwa ilitakiwa apewe kifungo cha kuanzia miaka mitano, sita na kuendelea.Hata hivy o mmoja wa watuwaliotoa maoni ya hukumu ya lulu alikuwa baba mzazi wa Kanumba ambae alisema kuwa adhabu aliyopewa msanii huyo ni kama adhabu ya kuua kuku tu.
Dr. Cheni amesema kuwa watu hao wamekuwa hawamtakii mema lulu na kusema kuwa jambo baya lolote linaweza kumpata mtu yeyote maana hakuna anaejua kesho yake, lakini pia amewashukuru wale wote waliomia na kutuma ujumbe wa pole kwa lulu pamoja na familia yake kwa ujumla.
Katika ukurasa wake wa instagram Dr.Cheni aliandika kuwa
Linapokukuta jambo wapo watakao kuonea huruma na wapo watakaokuwa na furaha ila niwakumbushe jambo hakuana anaejua kesho yake kubwa kila mapito mwambie mungu asante.watanzania tulio wengi wanakuombea yaliyo meme na tunakuhaidi tupo nyuma yako kukushika mkono kwa kila hatua maombi yao mungu atayasikia hata kama hukumu imepita tupo na wewe na mungu yuko na wewe.-aliandika Dr.Cheni
Lulu alipata hukuma yake tarehe 13 november mwaka huu baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia , maujia yalitokea April 2012 baada ya kugombana na mpenzi wake ambae pia alikuwa msanii wa bongo movie Steven Kanumba.
Pamoja na kwamba watu wengi wameonekana kuumia na hukumu hiyo lakini wapo walikuwa wakilalamika na kusema kuwa hukumu hiyo haiendani na maujia hayo.Baada ya hukumu ya lulu mengi yamesemwa kuhusu msanii huyo.
Maoni ya Dr.Cheni katika ukurasa wake wa Instagram