Dogo Janja Amwita Young Dee Teja
Ikiwa ni siku kadha zimepita na ugomvi kati ya wasanii wa Bongo Fleva Young Dee na Dogo Janja unazidi kuwa mzito huku kila mmoja akitaika kuwa juu zaidi ya mwenzie, ugomvi huu ambao ulianza kwa Young Dee kukataa kabisa kufananisha na wasanii wengine ambao hawapo kabisa katika level zake, kwa mujibu wa Young Dee anasema wasanii kama Dogo Janja wa Arusha na Young Killer wa Mwanza ni wadodgo sana katika swala la muziki na yeye ndie kaka yao hivyo kwanza wanapaswa kumheshimu lakini pia vyombo vya habari havipaswi kumfananisha wa wasanii hao.
Hata hivyo Dogo Janja ameamua kumjibu rapper huyo na kusema kuwa yeye hawezi kubishana na Young Dee kwa sababu Young Dee ni teja.Dogo Janja anasema kuwa ni sawa kabisa kwa Young Dee kukataa kufananishwa na yeye kwa sababau hata yeye pia hayuko tayari kabisa kufananishwa na Young Dee kwa sababu rapper huyo anatumia madawa ya kulevya na muda mwingi anaongea akiwa tayari ameshatumia madawa , na kutokana na matumizi ya madawa hayo ndio maana anaongea mambo ya ajabu ajabu”Young Dee ni mteja,na hawezi kufanana na mim.Mtu mwenye akili timamu hawezi kutukana kwenye Media matusi makubwa kama alivyofanya Young Dee, akiacha unga ndo ninaweza kuzungumza,siwezi jua kama saivi ntakuwa nazungumza au nabishana na yeye au na mteja.Mtu mwenye akili timamau unamsamehe tu maana inawezekana kashavuta mambo yake na yupo kwenye dunia yake nyingine” alifunguka Dogo Janja
Hata hivyo Dogo Janja anasema kuwa yeye hakatai kufananishwa na mtu lakini anaangalia mtu wa kufananishwa nae”mimi pia sipendi kufananishwa japo pia sikatai kufananishwa, Young Killer nilishawahi kuwa Role model wake kwaiyo kufananishwa nae si kitu kibaya lakini kufananishwa na mla unga ni kukosea.. Young Dee akiacha kula unga tutakaa mezani tuzungumze lakini kfananishwa nae kwa sasa hivi sitaki”
Baada ya Dogo Janja kuongea hivyo Young Dee alimjibu tena msanii huyo na kusema kuwa wao kama wasanii wadogo wanatakiwa wamfate yeye kaka yao ili wajue sababu ya yeye kusema hataki mkufananishwa nao,hata hivo Young Dee anasisitiza kuwa bila yeye wasanii wengine wadogo wasingekuwa hapo kimziki maana wote wamefunguliwa njia na yeye.