Dogo Janja Amuanika Hadharani Mpenzi Wake Mpya
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Abdul Chande maarufu kama Dogo Janja ameonekana kuendelea na maisha yake Baada ya kuachana na aliyekuwa mke Wake Irene Uwoya.
Dogo ameonekana akijiachia live na mwanamke mwingine anayetambulika kama Lina kwenye Mitandao ya kijamii ambapo walionekana wakiwa wanakumbatiana bila uwoga.
Wikiendi iliyopita Dogo Janja na mama yake mzazi walionekana kwenye party ya rafiki wa karibu wa Lina ambapo Dogo alikuwa anatumbuiza Lakini mara akaonekana akiwa anakumbatiana na Linah na mahaba hadharani.
Pamoja na taarifa za Dogo Janja kuwa kwenye mahusiano na linah Lakini Mpaka sasa hajathibitisha taarifa hizo.