Dogo Janja Amtuhumu Uwoya Kumgombanisha Na Mpenzi Wake
Kwa muda mrefu sana kumekuwa na tetesi za msanii wa muziki wa Bongo fleva Abdulazizi Chende maarufu kama Dogo Janja anaefanya vizuri kwa sasa na kibao chake cha Ngarenaro kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii wa Bongo movie Irene Uwoya. Pamoja na kukutana na mahojiano ya mara kwa mara na waandishi wa habari tofauti wawili hao hawajawahi kukubali hata kidogo kuwa wapo katika mahusiano ingawa pia wapo wanaosema kuwaona pamoja baadhi ya sehemu.
Katika wimbo wa Ngarenaro ambao Dogo Janja alitaja jina la Irene Uwoya , ilifanya watu wazidi kusema kuwa wawili hao wapo katika mahusuiano, lakini wao wenyewe wamekuwa wakikataa kabisa huku kwa uhalisia Dogo Janja anaonekana kuwa mdogo sana kwa Irene Uwoya kiumri, inawezekana hiyo pia inaweza kuwa ni sababu ya wawili ho kutotaka kuweka mahusiano yao wazi ingawa kwa sasa hivi wasanii wengi wa kike kutoka na wanaume wanaowazidi umri imekuwa ni kitu cha kawaida kabisa.
Hivyo Dogo Janja amefunguka na kusema tena kuwa hana mahusiano yoyote na msanii huyo wa bongo movie na tetesi za yeye kutembea na Irene Uwoya zimemletea mgogoro mkubwa sana kati yake na mpenzi wake aliyenae huku akudhani kuwa maneno hayo yanayosambaa katika mitandao yana ukweli ndani yake.
Sina mahusiano yoyote ya kimapenzi na irene uwoya, kwanza hii ishu imenileta ugomvi sana na mamlai wangu (mpenzi wake), ni stori ninzikia lakini sio ukweli,uwoya ni mshikaji wangu tu na tunawasiliana mara chache sana, lakini mapenzi nae sina.” alifunguka kwa undani Dogo Janja huku akitupia tuhuma izo kwa watu wanaozusha kuwa yeye naIrene uwoya wako katika mahusiano wanaharibu mahusiano na mwanamke aliyenae kwenye mahusiano kwa sasa.
Hitmaker huyo wa Ngarenalo kwa sasa amekuwa katika headline za vyombo vya habari kutokana na habari za mahusiano yake na msanii huyo wa kike lakini pia kutokana na bifu la chinichini lianloendelea kati yake na Young Dee ambapo wenyewe kwa wenyewe wamekuwa wakibishana kuhusu nani kuwa makli kuliko mwenzie na hakuna anaetaka kufananishwa na mwenzie.