Dogo Janja Amedai Hawezi Kumuacha Uwoya Kwasababu ya Picha Zake za Utupu na Tbway
Mwanamuziki wa Bongo fleva Dogo Janja amedai kuwa hawezi kumuacha mkewe Irene Uwoya kisa picha zake za utupu na Tbway.
Siku ya Jumapili Irene uwoya alizua tafrani mtandaoni baada ya picha kuvuja kwenye mitandaoni ya kijamii zilizomuonyesha akiwa amelala kitandani na mtangazaji wa East Africa Tv Tbway 360.
Picha ile ilizua utata kwa sababu ya staili ya ulalaji na wawili kutokuwa na nguo kabisa iliyoonyesha kabisa kuwa walikuwa ni zaidi ya marafiki kumaanisha ni wapenzi wa a in a Fulani.
Tendo hilo liliwashtua wengi kwa sababu ni mwezi tu umepita tangu Uwoya kafunga ndoa na mumewe Dogo Janja. Hivyo kwa mwanamke aliyeolewa kujiachia na mwanaume mwingine imekuwa kama usaliti.
Muda mfupi baadae habari zilisambaa kuwa picha zile zilikuwa za ukweli na haiku unganishwa kama watu wengi walivyokuwa wanadai lakini pia ilisemekana picha hizo zilikuwa za siku nyingi tangu wawili hao walipokuwa na uhusiano wa kimapenzi na sababu pekee iliyopelekea picha hizo kusambaa ni baada ya Simu waliyopiga picha hizo kuibiwa.
Baada ya sakata hilo Dogo Janja alifunguka kuhusu picha hizo na kusisitiza kuwa hawezi kumuacha mkewe, kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika:
Sigombani na mke wangu Kisa Jirani kasema nigombane naye!! Ntakuja naye Maisha club kumuimbia wimbo mzuri wa mapenzi na msisahau ikifika saa sita leo birthday yake kwaiyo karibu tumuimbie wote”.
Baada ya sakata hilo kutulia Tbway 360 amefunguka kwa kukiri kuwa picha zile ni yeye lakini zilikuwa picha za siku nyingi sana napia amemuomba radhi Dogo Janja na kudai kuwa anaheshimu ndoa ya Uwoya na Dogo Janja.