Dj Fetty Kurudi Radioni
Aliyewahi kuwa mtangazaji maaarufu wa Radio Clouds Dj Fetty inawezekana akarudi tena radioni na kuanza kufanya kazi katika radio moja wapo nchini baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu huku akitangaza kuwa alikuwa amestaafu kazi hiyo na kuamua kujikita katika biashara zake binafsi,
Dj Fetty amethibisha hayo katika ukurasa wae wa instagram akiwa kama anawadokeza kitu mashabiki wake kwa kuwaambia kuwa” Tizi imeanza , u want me back? weka comment yako zikifika 1000 mama la mama hewani”
Ingawa bado haijafahamika kama mwanadada huyo atarudi tena Clouds Fm au kuna sehemu nyingine anatarajia kufanya kazi lakini tetesi za chini ya kapeti ambazo hazijathibitishwa ni kwamba mwanadada huyo amajiriwa katika radio mpya ya Wasafi media.