Diva na Mpenzi Wake Heri Muziki Watoleana Povu Zito Baada ya Kukanana ‘Live’

Mtangazaji wa kipindi cha ‘Ala za roho’ cha Clouds Fm maarufu kwa sauti nyororo na vituko vyake Diva the Bawse ‘Loveness Malinzi’ ametoleana povu kali na mpenzi wake ambaye ni mwanamuziki wa RnB /Bongo fleva Heri Muziki.

Ugomvi wa wawili hawa ulianza live kwenye interview waliyofanya Clouds FM kupitia kipindi cha Leo tena ambapo walienda kwa ajili ya kuongelea kazi za kimuziki za Heri Muziki lakini katika maongezi wawili walichanganyana kwa sababu Diva alidai kuwa wao ni wapenzi na wanapendana sana lakini Heri alisema kuwa wameachana kwa sasa sio wapenzi tena ila wapo kikazi zaidi.

download latest music    

Baada ya interview kuisha wawili hao waliwashaiaba moto huku Diva akitaka majibu kwa nini amedhalilishwa kwa kukanwa redioni tena live bila chenga, baada ya hapo Diva aliingia Instagram na kuandika ujumbe mrefu wa kulalamika kudhalilishwa na mpenzi wake redioni na kutangaza kumuacha.

Baada ya sakata hilo wawili hao kila mmoja amefunguka kuhusu hali ilivyo kwa sasa na kujibu nini hasa kilichotokea.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo, Diva alizidi kufunguka yafuatayo:

Kuanzia sahivi sidhani kama naweza tena kumuita Heri Muziki mpenzi wangu kaniaibisha kanidhalilisha live kabisa angekuwa ananipenda asingefanya mambo kama yale mimi  nikaishia kuonekana kama najipendekeza kwake kwaiyo kuanzia Leo mimi najiona kama single girl alafu isitoshe hii haikuwa mara ya kwanza kanidhalilisha mbele za watu alishawahi kunitukana na kunidhalilisha tulipokuwa Arusha”.

Heri Muziki alipoulizwa na kuongelea tuhuma hizo alizotupiwa na mpenzi wake Diva amedai kuwa ameshangazwa na reaction yake wakati anajua fika kuwa kwa sasa hawana uhusiano wowote wa kimapenzi bali ni marafiki na wanafanya wote kazi hakuna kingine kinachoendelea zaidi ya hapo.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.