Dini Yamnyima Mo-Music Mchumba wa Kuoa.
Msanii wa muziki wa bongo, Moshi Katemi maarufu kama Mo Music jina la kisanii, amejikuta akiingia katika wakati mgumu wa kupoteza mwanamke wake wa kuoa na kunyanganywa mwanamke huyo na mwanaume mwingine kutokana na tofauti za kidini.
Mo Music ambae amekuwa katika mawazo ya muda mrefu na kukosa furaha alimpoteza mpenzi wake huyo wa siku wa nyingi aliyekuwa akijulikana kwa jina la Iptsam na walikuwa tayari wana mipango ya kuoana lakini baada ya kutokea mvutano wa kidini ndege huyo aliamua kupeperuka na kwenda kwai mwanaume mwingine anaendana nae kidini.
Akiongea na GPL, moja ya watu wa karibu wa Mo Music ambae ndio kilikuwa chanzo kikubwa cha habari hii alisema kuwa Mo Music alikuwa tayari ameshatoa mpaka mahari kwa wazazi wa mwanadada huyo nyumbani kwao lakini tatizo likaja katika dini kwa sababu Mo Music ni mkristo na mwanadada ni muislamu huku wote wakiwa hawajaridhika kutoka katika dini zao yaani hakuna akiyetaka kubadilisha dini na kumfuata mwenzake.
Baada ya kuvutana kwa muda mrefu binti huyo aliamua kuchumbiwa na mwanaume mwingine na kuolewa kabisa huku akimuacha Mo Muzic soremba bila hata kurudisha mahari.
Baada ya mwandishi kupata habari hIzo aliaamua kumtafuta moja kwa moja mhusika mkuu wa jambo hilo ambae ni mo muzic ili kujua ukweli wa tukio hilo.dah umenitonesha kidonda klichoanza kupoa, ni kweli kabisa kuwa demu yule kaolewa wiki iliyopita,kitendo cha kubadilisha dini kwangu kingewakera wazazi wangu, na ndio maana nikawa nasuasua na tupo kwenye mvutano waturudishie mahari yeti lakini wanauzungusha.-Alifunguka Mo-Music
Mo Music sasa hivi nafanya vizuri na wimbo wake mpya uliotoka hivi karibuni unaokwenda kwa jina la Kibajaji.