“Diamond Ruksa Amuoe Tanasha”- Lynn
Video vixen na msanii wa muziki wa Bongo fleva Irene Godfrey Louis amefunguka na kumpa baraka zote aliyekuwa mpenzi wake Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz kumuoa Mpenzi wake mpya Tanasha Donna Oketh.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Lynn ambaye aliwahi kutajwa kuwa mbioni kuolewa na Diamond alisema anawashangaa wanaosema anaumia juu ya kitendo cha Diamond kutangaza kumuoa Tanasha, jambo ambalo si kweli.
Sina kinyongo, Diamond amuoe Tanasha hata kesho maana ni jambo la heri. Ninafurahi sana kwa sababu Diamond ni mshkaji wangu sana na si vinginevyo”.
Diamond aliweka wazi mahusiano yake na mrembo Tanasha kutoka Kenya na kutangaza ndoa yao mara moja hali iliyopelekea taarifa kusambaa kuwa Lynn amemwaga na msanii huyo aliyekuwa kwenye mahusiano naye.